1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Starmer aanza kazi kwa kufuta mpango wa uhamiaji wa Sunak

7 Julai 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amesema anaifuta sera iliyo na utata ya mtangulizi wake Rishi Sunak, ya kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda.

Keir Starmer
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer Picha: Claudia Greco/AP Photo/picture alliance

Starmer ameapa kutekeleza matakwa ya wapiga kura ya uwepo wa mabadiliko nchini humo, lakini akatahadharisha kuwa kazi hiyo haitakuwa rahisi na haitofanyika haraka. Katika uchaguzi wa bunge uliomalizika, chama cha Starmer cha labour kilikishinda chama cha conservative chake waziri mkuu wa zamani Rishi Sunak, baada ya kuwa madarakani kwa miaka 14.

Akizungumza katika mkutano wake wa kwanza na waandishi habari katika ofisi yake ya Downing Street, Starmer amesema anataka sana mabadiliko lakini hawezi kuwaahidi waingereza ni kwa muda gani wataona mabadiliko katika viwango vyao vya maisha au huduma za ummah.

Keir Starmer awa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza

Serikali yake yenye mawaziri 25 , imeanza majukumu ikikabiliwa na  changamoto chungu nzima zikiwemo za kiuchumi, kisiasa, kuuboresha mfumo wa afya na kurudisha imani ya wananchi kwa serikali.