Serikali ya Syria yatangaza kusitisha mapigano Aleppo
9 Januari 2026
Katika taarifa yake, wizara hiyo imesema hatua hiyo inalenga "kuzuia kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi ndani ya maeneo ya makazi,” na hivyo kusitisha mapigano kuanza saa 9 alfajiri. Mapigano hayo yamekuwa yakihusisha vikosi vya serikali na vikosi vinavyoongozwa na Wakurdi vya SDF, ambapo watu wasiopungua 21 wameuawa katika siku kadhaa za makabiliano. Pande zote zinatupiana lawama kuhusu nani alianza mapigano hayo Jumanne, huku mazungumzo ya kuunganisha utawala na jeshi la Wakurdi na serikali yakikwama.Mapigano haya ambayo yanaripotiwa kuwa mabaya zaidi tangu mamlaka ya Kiislamu ichukue madaraka, pia zimeibua mvutano wa kikanda kati ya mshirika wa Damascus, Uturuki, na kwa upande mwingine Israel, ambayo imekemea kile ilichokiita mashambulizi dhidi ya Wakurdi.