SiasaUfaransa
Ufaransa yashikilia msimamo wake kuhusu mageuzi ya pensheni
19 Machi 2023Matangazo
Suala la utata katika mpango huo unaozingatiwa kuwa muhimu kwa Rais Emmanuel Macron ni juu ya kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64.
Hapo jana maelfu ya wananchi wa Ufaransa walifanya maandamano makubwa ya kuupinga mpango huo wa mageuzi. Polisi walifunga eneo la "La Concorde" lililo mkabala na Bunge. Jumla ya watu 169 walikamatwa kote Ufaransa kufuatia maandamano hayo.
Soma zaidi: Ufaransa yakabiliwa na maandamano zaidi kuhusu sheria ya pensheni
Maandamano hayo yamepelekea wafanyakazi wa jiji kusitisha ukusanyaji wa taka katika sehemu kubwa ya jiji la Paris, ambako takriban tani 10,000 za taka zimetapakaa mitaani huku serikali ikiwalazimisha baadhi ya wazoa taka kurejea kazini.