Serikali ya Uganda na kundi la LRA wakubaliana kurejea katika meza ya mazungumzo
17 Aprili 2007Matangazo
Kwa mujibu wa msemaji wa kundi hilo kiongozi wa LRA Joseph Kony alishuhudia kutiwa saini makubaliano hayo katika eneo la Ri-Kwangba nchini Sudan. Joseph Kony anachelea kuonekana kwa kuhofia kukamatwa na kupelekwa The Hague Uholanzi ili kujibu mashtaka ya kuhusika na uhalifu wa kivita. Pande zote mbili zilitia makubaliano ya amani mwezi Agosti na mazungumzo kukwamishwa na vitendo vya uhasama.
Mwandishi wetu Omar Mutasa anaarifu zaidi kutoka Kampala.