1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatma ya sera ya wahamiaji kwenda Rwanda kuamuliwa Uingereza

15 Novemba 2023

Mahakama ya Juu nchini Uingereza itatoa uamuzi iwapo sera tata ya serikali ya kuwapeleka wahamiaji Rwanda ni halali kisheria au la.

Großbritannien | Protest gegen das Gesetz über Nationalität und Grenzen in London
Picha: Thomas Krych/Zuma Press/picture alliance

Uamuzi huo unatarajiwa kuwa na athari kubwa kisiasa kwa Waziri Mkuu Rishi Sunak.

Kiongozi huyo wa chama cha Conservative anasema mpango huo ni muhimu kwa kupunguza uhamiaji unaoongezeka, suala ambalo linatarajiwa kuwa mada muhimu ya mapambano katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwaka ujao.

Mahakama Uingereza kusikiliza hoja kupeleka wahamiaji Rwanda

Majaji watano watatangaza uamuzi wao kuhusu ombi la serikali linalopinga hukumu ya mahakama ya chini iliyosema kuwa sera hiyo ni kinyume cha sheria.

Uamuzi mzuri unaweza kuongeza nafasi ya Sunak kupambana na chama kinachopata umaarufu mkubwa cha Labor, lakini akishindwa basi mipango yake ya uhamiaji itasambaratika.

Mpango wa UK kuwapeleka wahamiaji Rwanda waenda mahakamani

Hilo pia linaweza kuongeza mipasuko katika chama tawala cha Conservative kati ya wabunge wa mrengo wa kulia na wa siasa za wastani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW