1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Uingereza yaidhinisha kuuzwa kwa Chelsea FC

25 Mei 2022

Serikali ya Uingereza imesema leo kuwa imetoa idhini kwa mfanyibiashara Todd Boehly kuinunua klabu ya Chelsea kutoka kwa mmilki wake wa sasa aliyewekewa vikwazo Roman Abramovich.

FC Chelsea
Picha: Nick Potts/PA/empics/picture alliance

Waziri wa utamaduni, habari na michezo wa Uingereza Nadine Dorries amesema ametoa leseni inayoruhusu kuuzwa kwa klabu hiyo jana Jumanne, muda mfupi tu baada ya kupata idhini kutoka kwa wasimamizi wa ligi kuu ya Premia.

Dorries aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa, wameridhika kwamba mapato yanayotokana na kuuzwa kwa klabu hiyo hayatamnufaisha Roman Abramovich ama watu wengine karibu yake waliowekewa vikwazo kutokana na uhusiano wao na mamlaka nchini Urusi.

Kampuni inayosimamiwa na Boehly, ambayo pia inamiliki klabu ya mpira wa Marekani ya Los Angeles Dodgers, ilikubali dau la pauni bilioni 4.25 la kuinunua Chelsea mnamo Mei 7.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW