Ujerumani yaidhinisha bajeti ya ziada kuepusha mgogoro
27 Novemba 2023Serikali ya KanselaOlaf Scholz iliingia kwenye mgogoro wa bajeti baada ya kulazimika kusitisha bajeti ya kusimamia miradi mingi mipya, kufuatia uamuzi wa mahakama ya katiba wa kuizuia hatua yake ya kutaka kutumia fedha zilizobakia wakati wa janga la Corona katika miradi ya mazingira pamoja na kutoa ruzuku kwa viwanda.
Serikali ya Ujerumani inapambana kujikwamua kutoka kwenye mgogoro ambao umechochea kutolewa tahadhari kuhusu ukuaji wa kiuchumi na kuondoka kwa wenye viwanda.
Soma pia:Rungu la Mahakama latikisa sehemu ya bajeti ya Ujerumani
Kiongozi maarufu wa upinzani wa chama cha kihafidhina kutoka jimbo la Bavaria, Christian Social Union-CSU, Markus Söder amesema serikali hiyo ya mseto inapaswa kuitisha uchaguzi wa mapema,akidai imepoteza uwezo wa kuyatatua matatizo ya nchi.