UchumiUjerumani
Serikali ya Ujerumani yalumbana juu ya bajeti
20 Juni 2024Matangazo
Waziri wa Fedha Christian Lindner anayetoka chama cha Waliberali, FDP anataka serikali ibanie kiasi cha takriban Euro bilioni 30. Vyama vingine vilivyomo katika serikali hiyo, vya Kijani na Social Demokratic, SPD vinapinga.
Wajumbe wa serikali hiyo ya pande tatu wanao muda wa hadi tarehe 3 Julai ili kufikia mwafaka. Serikali ya mseto ya Ujerumani imekuwa inakabiliwa na mivutano juu ya masuala kadhaa mnamo miezi ya hivi karibuni.
Wataalamu wanasema mzozo huo wa bajeti unaweza kuisambaratisha serikali ya mseto. Kulingana na taarifa ya wizara ya fedha, mapato ya kodi yanatarajiwa kupungua kwa Euro bilioni 11 mwaka ujao.