Serikali ya Ujerumani yapata mwafaka kuhusu bajeti ya 2024
13 Desemba 2023Matangazo
Hii ni kufuatia mazungumzo ya wiki kadhaa, baada ya uamuzi wa mahakama mwezi uliopita uliotupilia mbali makadirio hayo na kuzusha mtafaruku.
Kulingana na vyanzo vitatu vya serikali ambavyo vimezungumza na shirika la habari la Reuters mapema leo, serikali itawasilisha makadirio hayo ya bajeti baadaye leo bungeni.
Mnamo Novemba 15, mahakama ya kikatiba ya Ujerumani iliamua kwamba uamuzi wa serikali kutenga euro bilioni 60 ya deni ambalo halikutumika katika janga la COVID-19, kuelekeza kwenye Mfuko wake wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ulikuwa kinyume na katiba.