Serikali ya umoja wa kitaifa kutangazwa hivi punde huko Lebanon
5 Julai 2008Matangazo
Beirut
Waziri wa michezo na masuala ya vijana nchini Lebanon Ahmed FatFat amesema wakati wowote kutoka sasa serikali ya umoja wa kitaifa itatangazwa ikiwa ni wiki sita baada ya kufikiwa makubaliano kati ya vyama vinavyopingana.Waziri huyo ambaye alikuwa na mazungumzo na rais Micheil Suleiman mapema hii leo amesema vyama vya kisiasa nchini humo vimefahamu kuwa hali iliyoko sasa ya mkwamo juu ya kuundwa serikali haiwezi kuendelea lakini hakutoa maelezo juu ya vipi suala linalohusu ugavi wa madaraka lilivyotatuliwa.