1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Yevgeny Prigozhin afariki dunia

27 Agosti 2023

Kamati ya uchunguzi ya nchini Urusi hatimaye imethibitisha kifo cha aliyekuwa kiongozi wa kundi la mamluki wa kijeshi la Wagner, Yevgeny Prigozhin.

Mamlaka za Urusi haytimaye zathibitisha kwamba kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner evgeny Prigozhin amefariki dunia.
Yevgeny Progozhin atakumbukwa kwa uwezo wake wa kumkabili rais Vladimir Putin wa Urusi bila ya uwoga.Picha: Alexander Zemlianichenko/AP/picture alliance

Hii ni baada ya siku kadhaa ya minong'ono kwamba kiongozi huyo alifariki katika ajali ya ndege iliyokuwa imewabeba abiria kumi, ikitokea Moscow kueleka St. Petesburg.

Kamati hiyo imethibitisha kifo hicho baada ya vipimo vya kijenetiki kushabihiana na abiria 10 waliokufa kwenye ajali hiyo, ambao ni pamoja na Prigozhin.

Mamlaka ya anga ya Urusi mapema wiki hii ilisema Prigozhin pamoja na baadhi ya maafisa wake walikuwa katika orodha ya wale waliopanda ndege hiyo iliyoanguka siku ya Jumatano.

Soma Pia: Je, kifo cha Prigozhin kitamuimarisha Putin?

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW