1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Serikali ya Venezuela yatangaza siku saba za maombolezo

7 Januari 2026

Venezuela imetangaza wiki moja ya kuwaomboleza wanajeshi waliouawa katika shambulio la Marekani. Cuba pia yatangaza siku mbili za kuwaomboleza wanajeshi waliouawa nchini Venezuela.

Venezuela Caracas 2026 | Mazishi ya mtu aliyeuawa kwenye mashambulizi ya Marekani nchini Venezuela
Mazishi ya mmoja wa watu aliyeuawa kwenye mashambulizi ya Marekani nchini Venezuela ambako Kiongozi Nicolas Maduro alitekwaPicha: Gaby Oraa/REUTERS

Serikali ya mpito ya Venezuela hii siku ya Jumanne imetangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa kwa ajili ya kutoa heshima na kuwakumbuka wanajeshi waliouawa katika shambulio la Marekani katika mji mkuu wa Caracas ambako kiongozi wa Venezuela Nicolás Maduro alitekwa.

Kaimu Rais Delcy Rodríguez amesema kwenye televisheni ya taifa kwamba wanajeshi 24 wa Venezuela waliuawa katika shambulio hilo la Marekani, lililofanywa mapema siku ya Jumamosi.

Katikati: Kaimu Rais wa Venezuela Delcy RodríguezPicha: Jesus Vargas/Getty Images

Huko nchini Cuba majina, vyeo na umri wa wanajeshi 32 wa nchi hiyo waliouawa wakati wa kutekwa Kiongozi wa Venezuela Nicolás Maduro yamechapishwa na serikali ya nchi hiyo na imetanga siku mbili za maombolezo.

Huko Marekani utawala wa Trump umesema umemweka waziri wa mambo ya ndani wa Venezuela mwenye msimamo mkali Diosdado Cabello, katika orodha yake ya walengwa wakuu labda alegeze msimamo wake na akubali kumsaidia Rais wa mpito Delcy Rodriguez kukidhi mahitaji ya Marekani na kuweka utulivu nchini Venezuela baada ya kutekwa Nicolas Maduro.

Cabello, ambaye ni mkuu wa vikosi vya usalama vinavyoshutumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ni mmoja wa wafuasi wachache wa Maduro ambao Rais Donald Trump ameamua kuwategemea kama watawala wa muda ili kudumisha utulivu wakati wa kipindi cha mpito.

Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Alex Brandon/AP Photo/dpa/picture alliance

Mengineyo rais Trump amesema serikali ya mpito ya Venezuela itakabidhi kati ya mapipa milioni 30 hadi milioni 50 ya mafuta yaliyokuwa yamewekewa vikwazo hatua aliyoitaja kuwa itanufaisha mataifa yote mawili.

Katika chapisho kwenye jukwaa lake la Truth Social, Trump amesema mafuta hayo yatauzwa kwa bei iliyopo kwenye soko la kimataifa na kwamba yeye atadhibiti mapato ya mafuta hayo ili kuhakikisha fedha zinatumika kuwanufaisha watu wa Venezuela na Marekani.

Amesema makampuni makubwa ya mafuta ya Marekani yatawekeza mabilioni ya dola kwa ajili ya kutengeneza miundombinu na kuendeleza uzalishaji wa mafuta nchini Venezuela.

Kiongozi wa upinzani wa Venezuela María Corina MachadoPicha: Ole Berg-Rusten/NTB/dpa/picture alliance

Naye Kiongozi wa upinzani wa Venezuela na mshindi wa hivi karibuni wa Tuzo ya Amani ya Nobel María Corina Machado amesema yuko tayari kuwatumikia watu wa Venezuela. Machado amesema yuko tayari kuongoza nchi yake licha ya kutengwa na utawala wa Trump.

 

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW