1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali zafungua shughuli,WHO yaonya kuhusu wimbi la pili

Sekione Kitojo
12 Mei 2020

Janga la virusi vya corona limewauwa  zaidi ya watu 285,000 duniani kote, kwa mujibu wa  data za shirika  la  habari  la  Ufaransa AFP, huku idadi ya  maambukizi ikifikia  watu  milioni 4.1.

Filmstill Corona-Chroniken | Koproduktion DW, Arte & rbb | Majdi Arsanjani
Picha: Berlin Producers

Wakati shughuli zimeanza kufunguliwa tena katika  nchi mbali  mbali shirika la  afya ulimwenguni WHO linaonya  kuhusu hatari ya  wimbi  la  pili la  maambukizi.

Wafanyakazi ya huduma ya usafiri mjini Paris waliovalia vizuwizi usoni na barakoa wako nje ya kituo cha treni wakichukua hatua ya kuwatahadharisha wasafiri kufuata sheria ya kuzuwia maambukiziPicha: AFP/G. van der Hasselt

Marekani imeingia  siku  ya  pili  ikiwa  na  vifo vichache ambapo ni watu 900 waliofariki, wakati shirika  la  afya ulimwenguni WHO likisifu hatua za maendeleo  zilizopigwa duniani  lakini  limeonya kuwa  na  haja  ya  kuchukua  tahadhari  ya  hali  ya  juu, dhidi  ya kile  ilichosema  kuwa  ni  wimbi  la  pili la  maambukizi.

Matumaini yamechafuliwa  na  hali  mbaya  inayoongezeka ya uchumi, ambapo Ufaransa  inaonesha  kuanguka  kwa  kiasi  kikubwa kwa  shughuli  mwezi uliopita na  kuonya  kuwa  shirika  kubwa  la ndege  la  Marekani  huenda  likafilisika kwasbabu  ya  janga  hili, huku  nafasi  za  kazi  zikipotea na  biashara  kuporomoka.

Kiwango cha  maambukizi  katika  nchi  nyingi  kimeanza  kupungua, shirika  la  afya  ulimwenguni WHO limeeleza, mbapo wiki  kadhaa za  kuwazuwia  watu  kutoka  nje  zimezaa  matunda.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom GhebreyesusPicha: Getty Images/AFP

Wimbi la pili la maambukizi

"Taarifa  nzuri  ni  kwamba  kumekuwa  na  mafanikio  makubwa katika  kupunguza  kasi  ya  maambukizi  na  hatimaye  kuokoa maisha," mkurugenzi  mkuu wa  WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliuambia  mkutano kwa  njia  ya  vidio.

Lakini  shirika  hilo  la  afya  ulimwenguni limeonya  kuhusu  kutokea kwa  wimbi la  pili la  maambukizi, ambapo mkuu  wa  kitengo  cha dharura  Michael Ryan  amelalamika kwamba  baadhi  ya  serikali zinachagua "kutembea  kama  vipofu" kwa  kutoongeza  uwezo wa kufanya  uchunguzi  na  kufuatilia watu waliokutana  na  wale walioambukizwa.

Virusi  vinaonekana  kuingia  katika  Ikulu  ya  Marekani  ya  White House mwishoni  mwa  juma, ambapo kumekuwa  na  mtu  wa  pili aliyethibitishwa  kuwa  na  virusi  hivyo. Wafanyakazi  katika  Ikulu ya  White House  wameamriwa  kuvaa  barakoa kazini, na  rais Donald Trump  amesema  huenda  akapunguza  kukaribiana  na  watu baada  ya  msaidizi wa  makamu  wa  rais Mike Pence  kugundulika kuwa  ana  virusi  vya  corona.

Makamu wa rais wa Marekani Mike PencePicha: Getty Images/W. McNamee

Mtandao  wa  reli  nchini  India  unanza  kufanyakazi  leo wakati  nchi hiyo taratibu  ikiondoa  hatua za  kuwazuwia  watu  kutoka majumbani  mwao , licha  ya  kuwa  maambukizi  mapya yanaongezeka.

Nchi hiyo  yenye  wakaazi bilioni 1.3 iliweka hatua  kali za  kuwataka watu kutotoka  nje mwishoni  mwa  mwezi Machi, wakati serikali  ya waziri  mkuu Narendra Modi imsifiwa  kwa  kufanikiwa kubakisha idadi  ya  walioambukizwa  kuwa  70,000, na  vifo 2,000, tu.

Japan imethibitisha  kuwa  na  kesi  mpya za  maambukizi 28 leo, ikiwa  ni  siku  ya  saba  mfululizo  ambapo idadi  ya  kila  siku imebakia  chini  ya  watu 40.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW