1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Shambulio la anga lawaua raia 20 huko Sudan

Sylvia Mwehozi
3 Septemba 2023

Wakaazi wa mji mkuu wa Sudan wa Khartoum wametikiswa na milio ya mizinga na maroketi, saa chache baada ya shambulio la anga katika eneo la kusini mwa mji huo kuwaua watu 22 wakiwemo watoto wawili.

Sudan
Wakimbizi wa Sudan waliokimbia mapiganoPicha: Marie-Helena Laurent/WFP/AP/picture alliance

Wakaazi wa mji mkuu wa Sudan wa Khartoum wametikiswa na milio ya mizinga na maroketi, saa chache baada ya shambulio la anga katika eneo la kusini mwa mji huokuwaua watu 22 wakiwemo watoto wawili.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa kundi moja la wanaharakati wa Sudan ambalo lilikuwa miongoni mwa makundi yaliyoandaa maandamano ya kudai demokrasia na kutoa usaidizi kwa familia zilizonasa kwenye mapigano baina ya makamanda wawili.

Awali, wanaharakati hao walionya kwamba vifo vingi havijarekodiwa kwani miili ya wahanga haikuweza kupelekwa hospitali kwasababu ya kuchomeka vibaya au kukatwa katwa vipande katika mlipuko huo.

Tangu vita ianze kati ya jeshi na kikosi cha wanamgambo wa RSF katikati ya mwezi wa nne, watu wapatao 5,000 wameuawa kwa mujibu wa takwimu za shirika moja linalofuatilia mizozo na data.