1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Shambulio la droni ya Urusi lauwa watu wawili Ukraine

Hawa Bihoga
2 Machi 2024

Watu wawili wameuwawa, wanane kujeruhiwa na wengine sita hawajulikani walipo baada ya droni ya Urusi kuanguka kwenye jengo la makaazi katika mji wa bandari wa Odesa, kusini mwa Ukraine.

Ukraine | Rais  Wolodymyr Selensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akiongea kutoka mstari wa mbele wa vitaPicha: Ukrainian Presidential Press Service/REUTERS

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kupitia mtandao wa Telegram, amesema vikosi vya Urusi vimeendelea kupigana dhidi ya raia na kuongeza kuwa shambulio hilo la droni limeharibu nyumba 18 za makaazi.

Gavana wa mji wa Odesa Oleh Kiper, amesema zoezi la kutafuta manusura katika vifusi bado linaendelea na tayari mtu mmoja ameokolewa akiwa hai na kuna uwezekano alikuwa katika chumba cha ardhini wakati wa shambulio.

Soma pia:Putin asifu mafanikio Ukraine, atishia vita vya nyuklia

Katika siku za hivi karibuni Urusi imeonekana kusonga mbele kwenye uwanja wa vita, wakati Ukraine bado ikiendelea kusaka msaada zaidi wa kijeshi kutoka kwa washirka wake nchi za Magharibi.