Shambulio la Gruneti mjini Garissa
5 Novemba 2012Matangazo
Hali ya usalama katika eneo hilo imekuwa tete tangu majeshi ya Kenya kungia katika mipaka ya Somalia kwa lengo la kuwasaka wanamgambo wenye mafungamano na al-Qaeda, al-Shabaab. Mkasa huu wa sasa kutokea unafuatia ule mwingine wa guruneti ulitokea Julai na kusababisha vifo vya watu 18. Kutoka mjini Nairobi Sudi Mnette amezungumza na Naibu Msemaji wa Jeshi la Polisi wa Kenya, Charles Owino na kwanza amenielezea kipi wanachofanya sasa katika eneo la Garissa ambalo wakaazi wake wengi ni jamii ya watu wenye asili ya kisomali.
(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri:Yusuf Saumu