1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Shambulio la kisu lazusha vurugu Ireland Kaskazini

10 Juni 2026

Waandamanaji wanaopinga wahamiaji wamechoma moto majengo na magari kwenye mji mkuu wa Ireland Kaskazini, Belfast siku moja baada ya kutokea shambulio la kisu linalodaiwa kufanywa na mhamiaji kutoka Sudan.

Ghasia zilizoshuhudiwa Ireland Kaskazini.
Ghasia zilizoshuhudiwa Ireland Kaskazini. Picha: Isabel Infantes/REUTERS

Shirika la Habari la AFP limeripoti kwamba mamia ya waandamanaji waliojifunika nyuso walikusanyika kwenye maeneo kadhaa ya mji wa Belfast wakirusha mabomu ya petroli na kufunga barabara.

Basi la abiria na magari kadhaa yamechomwa moto huku jengo moja nalo lilishika moto na kulazimisha wakaazi wake kuondolewa. Tukio lililochochea vurumai hiyo lilirekodiwa kwenye video na taarifa zinasema mtuhumiwa wa shambulio hilo kisu tayari amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua.

Wanasiasa na wanaharakati wanaopinga uhamiaji wanataka jina lake litajwe baada ya wizara ya mambo ya ndani kuthibitisha anayetuhumiwa ni mhamiaji kutoka nchini Sudan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW