1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la Urusi lalaumiwa kimataifa.

6 Desemba 2003
BERLIN/WASHINGTON: Lile shambulio la treni la kujitolea mhanga maisha huko Urusi ya Kusini limelaumiwa vikali kimataifa. Katika risala yake kwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani alisema amesikitishwa sana na kitendo hicho cha kikatili. Katika risala yake hiyo, Kansela Schröder amewapa mkono wa rambi rambi jamaa wa watu waliouawa katika shambulio hilo. Nayo serikali mjini Washington ilisisitiza kuwa hapakuwa na sababu yoyote ya kufanywa shambulio kama hilo na kwamba Marekani inalaumu kila aina ya ugaidi. Naye Katibu Mkuu wa UM, Kofi Annan alisema amesikitishwa sana na kitendo hicho cha kikatili. Ugaidi hauwezi kukubalika kwa hali yoyote, alisema kutoka makao yake makuu mjini New York.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW