1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la Urusi laua wanne Ukraine

11 Februari 2026

Mji wa Bogodukhiv ni miongoni mwa maeneo ya Ukraine ambayo kwa siku za hivi karibuni yamekuwa yakilengwa na mashambulizi ya Urusi hasa katika sehemu za miundombinu ya usafiri na nishati.

Ukraine I 2024
Moja ya uharibifu uliotokana na shambulio la anga la Urusi nchini UkrainePicha: Pressedienst der Staatsanwaltschaft von Donezk Oblast

Maafisa nchini Ukraine wamesema leo kwamba shambulio la Urusi katika mji wa Bogodukhiv mashariki mwa nchi hiyo limewaua watu wanne, wakiwemo watoto watatu.

Akiutumia mtandao wa kijamii wa Telegram, Mkuu wa jeshi katika mji huo Oleg Synegubov amesema shambulio hilo la anga la Urusi liliilenga nyumba moja na kuwaua watu hao.

Mji wa Bogodukhiv ni miongoni mwa maeneo ya Ukraine ambayo kwa siku za hivi karibuni yamekuwa yakilengwa na mashambulizi ya Urusi hasa katika sehemu za miundombinu ya usafiri na nishati.

Kulingana na Ujumbe wa Ufuatiliaji wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine ni kwamba takriban watu 15,000 wameuawa tangu Urusi ilipoivamia nchi hiyo Februari 2022. Na licha ya juhudi mbalimbali za kuvimaliza vita hivyo vya karibu miaka minne bado nchi hizo mbili zimeendelea kushambuliana.  
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW