1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahothi waishambulia meli moja katika Bahari ya Shamu

Sylvia Mwehozi
15 Machi 2024

Shambulio linaloshukiwa kufanywa na waasi wa Kihouthi wa Yemen, limeipiga meli moja kwenye Bahari ya Shamu mapema leo na kusababisha uharibifu kidogo kwenye meli hiyo.

Yemen I Houthi
Mmoja ya mwanachama wa waasi wahouthi nchini YemenPicha: Mohammed Hamoud/Anadolu/picture alliance

Shambulio hilo lililotokea nje ya mji wa bandari wa Hodeida, ni mwendelezo wa kampeni ya mashambulizi yanayofanywa na Wahouthi dhidi ya meli za kibiashara, kupinga vita vinavyoendelea vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Kitengo cha operesheni za biashara ya Baharini ya jeshi la Uingereza, kimeeleza kwamba wafanyakazi wako salama na meli imeendelea na safari yake, ikiashiria kwamba uharibifu haukuwa mkubwa.

Marekani yashambulia maeneo ya Wahotuhi wa Yemen

Kampuni binafsi ya usalama ya Ambrey pia imethibitisha shambulio hilo na kudai kwamba meli hiyo hapo awali ilikuwa na uhusiano na Israel lakini ilibadili wamiliki wake mwezi Februari. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW