1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio nchini Ufaransa limeleta hofu Ujerumani pia

9 Januari 2015

Huenda ni ubinadamu unaotusukuma katika hali hii, kwamba baada ya mshituko, hasira, na majonzi kuhusiana na shambulio la kigaidi dhidi ya jarida la dhihaka la Charlie Hebdo, hata hapa ujerumani ulinzi umeongezwa.

Frankreich Anschlag auf Charlie Hebdo Karikatur
Maandamano ya kupinga shambulio dhidi ya jarida la "Charlie Hebdo"Picha: Getty Images/D. Kitwood

Msako bado unaendelea kuwatafuta ndugu wawili wanaoshukiwa kufanya shambulio nchini Ufaransa dhidi ya wafanyakazi wa jarida la Charlie Hebdo.

Baadhi ya magazeti yameongeza ulinzi katika maeneo yao. Hususan kwa upande wa waandishi, ambao hapo kabla wametumia katuni za kudhihaki zilizochapishwa na jarida hilo la "Charlie Hebdo".

Jeshi la usalama limewekwa kila mahali nchini Ufaransa kuwasaka washambuliajiPicha: Reuters/C. Hartmann

Hali hiyo inakuja wakati baada ya maafisa wa usalama kufanya tathmini yao kutokana na shambulio lililotokea nchini Ufaransa , kitisho nchini Ujerumani pia hakujabadilika.

Hatari bado ya juu nchini Ujerumani

Hatari ya kutokea shambulio la kigaidi inaweza kuelezwa kuwa bado ni ya juu. Hata hivyo hakuna taarifa juu ya uwezekano wa kutokea shambulio.

Kuzuwia shambulio kama lililotokea nchini Ufaransa si rahisi, anaelezea katika tathmini yake mtaalamu wa wa masuala ya uhalifu Andreas Armborst kutoka chuo kikuu cha Leeds nchini Uingereza.

Kwa kuwa wapo magaidi, ambao wako tayari kufanya uhalifu huo, inawezekana kabisa katika jamii yenye uhuru kuwapo na uwezekano huo, kwa hiyo kutakuwa na mtu wa aina hiyo ambaye anaweza kuchukua hatua kama hiyo, ameeleza Armborst katika mazungumzo na DW.

Shambulio dhidi ya jarida la Charlie Hebdo nchini UfaransaPicha: Getty Images/P. Le Segretain

Hadi sasa ni shambulio moja tu la Waislamu wenye itikadi kali lililotokea nchini Ujerumani ambapo maisha ya watu yamepotea.

Machi , 2011 Mualbania mwenye asili ya Kosovo aliwapiga risasi wanajeshi wawili wa Marekani katika uwanja wa ndege wa Frankfurt.

Hata hivyo kuna majaribio mengi ya mashambulio yaliyotokea. Majaribio hayo ama yameshindwa ama yamegunduliwa kabla.

Hatari inaongezeka pamoja na ongezeko la matukio ya Waislamu.

Kundi la Salafisti ni hatari zaidi

Hususan hatari inaongezeka zaidi kutokana na kundi ambalo linaimani za kihafidhina zaidi la Salafi.

Idadi yao imeongezeka maradufu kutoka idadi inayoaminika kuwa watu 7,000. Na hasa kama wanavyoeleza wataalamu wa masuala ya usalama ni wanaporejea kutoka katika vita nchini Syria na Iraq baadhi ya wapiganaji.

Tarakimu rasmi zinasema kuwa wako wapiganaji 600 wenye itikadi kali katika eneo hilo la vita ambao wako katika kile kinachojulikana kama Dola la Kiislamu.

Wanaharakati wa kundi la Salafisti wakigawa vitabu vya Koran nchini UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa/J. Stratenschulte

Baadhi ya wachunguzi , kama mtaalamu wa masuala ya saikolojia na wataalamu wanaoangalia hali ya Uislamu Ahmad Mansour anaeleza kuwa wako Wajerumani 1,500 hadi 2,000 wanaopigana jihadi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

Kiasi ya watu 180 waliokwenda nchini humo wamerejea nchini Ujerumani.

Mtafiti kuhusu itikadi kali Peter Neumann kutoka chuo kikuu cha mjini London cha Kings anatofautisha makundi matatu ya wale waliorejea, ambayo yana uhusiano tofauti pia.

Baadhi ya wapiganaji wa jihadi ni hatari

Kiasi ya asilimia 10 ya kundi la watu hao anasema Neumann , ni hatari sana, wana uwezo wa kuchukua hatua za kigaidi wakati wakirejea. Na hawa ni watu , ambao kwa utaratibu jamii inapaswa kulinda dhidi yao. Ni kundi ambalo linapaswa kufuatiliwa kwa karibu na kuadhibiwa kwa kufungwa jela. Kundi la pili ni lile lililoathirika na kupata fadhaa na kwa kiasi fulani kuathirika kiakili. Kundi hili anasema Neumann kuwa linapaswa kupatiwa uangalizi wa kisaikolojia ama kiakili.

Maandamano ya kupinga kusambaa kwa Uislamu nchini Ujerumani "PEGIDA"Picha: Reuters/H. Hanschke

Kundi la tatu anasema mtaalamu huyo kuwa ni wale wasio ridhika baada ya kutoka Syria. Mmoja kati ya vijana hao ndugu wenye asili ya Algeria , ambao wanatuhumiwa kufanya shambulio dhidi ya wafanyakazi wa jarida la Charlie Hebdo, ni wapiganaji wa jihadi wanaotokea nchini Iraq. Kabla ya hapo mwaka 2008 alihukumiwa kwenda jela miaka mitatu, ambapo alitumikia miezi 18. Msimamo wake haukubadilika. Inawezekana kwamba jela imemzidishia zaidi itikadi yake kali, anafafanua mtaalamu wa masuala ya usalama Raffaelo Pantucci kutoka London.

Mwandishi: Hein, Matthias / ZR/ Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo