1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKenya

Shambulizi la Al-Shabaab lawauwa watu 4 Kenya

26 Machi 2024

Watu 4 wakiwemo maafisa watatu wa polisi wameuwawa katika shambulizi linaloshukiwa kufanywa na wanamgambo wa Al-Shabaab katika mji mmoja wa Kenya uliopo karibu na mpaka wa Somalia.

Mafisa wa polisi ya Kenya wakipiga doria mitaani
Mafisa wa polisi ya Kenya wakipiga doria mitaaniPicha: Billy Mutai/SOPA/ZUMA/picture alliance

Kwa mujibu wa polisi, kulitokea mlipuko katika hoteli moja karibu na kituo cha polisi mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya, eneo ambalo kwa kawaida hulengwa sana na wanamgambo hao.

Polisi inasema watu wengine kadhaa wamejeruhiwa kutokana na shambulizi hilo. Vyombo vya habari nchini Kenya vinaripoti kuwa maafisa wengine wawili wa polisi wa akiba waliuwawa katika uvamizi wa mwishoni mwa wiki iliyopita uliofanywa na wanamgambo hao katika Kaunti ya Lamu, kaskazini mwa Kenya.

Taifa hilo la Afrika Mashariki ni mchangiaji mkubwa wa wanajeshi kwenye kikosi cha Umoja wa Afrika kinachoiunga mkono serikali kuu ya Somalia katika mapambano yake dhidi ya Al-Shabaab, na kwasababu hiyo limekabiliwa na mashambulizi kadhaa hatari ya kulipiza kisasi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW