1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaPakistan

Shambulizi la Bomu laangamiza maisha ya watu 52 Pakistan

29 Septemba 2023

Takriban watu 52 wamekufa na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa hii leo nchini Pakistan, kufuatia shambulio la kujitoa mhanga.

Athari za shambulizi la kujitoa mhanga Bajaur, Pakistan
Mashambulizi ya kujitoa mhanga hutokea mara kwa mara nchini Pakistan, taifa linalokabiliwa na makundi ya wapiganaji wa itikadi kali. Mathalan picha hiyo hapo juu inaonesha athari za shambulio la kujitoa mhanga lililotokea mwezi Julai, 2023 huko Bajaur, Pakistan.Picha: Bilal Yasir via REUTERS

Shambulio hilo limetokea wakati wa sherehe za kidini huko Mastung katika mkoa wa kusini magharibi wa Baluchistan, wakati waumini wa Kiislamu wakisherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad.

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi eneo hilo Munir Ahmed ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa mshambuliaji alijilipua karibu na gari la Naibu Msimamizi wa jeshi la Polisi lililokuwa limeegesha karibu na msikiti uliobomoka na kuwafukia chini ya vifusi watu wengine kati ya 30 na 40.

Hadi sas hakuna kundi lililodai kuhusika na mlipuko huo ambao inajiri huku kukiwa na ongezeko la mashambulizi ya makundi ya wapiganaji magharibi mwa Pakistan, hali inayozidisha changamoto kwa vikosi vya usalama kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Januari mwakani.