1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la droni la Urusi lawauwa watu wawili Ukraine

7 Juni 2026

Maafisa nchini Ukraine wamesema, mashambulizi ya droni ya Urusi hii leo yamesababisha vifo vya watu wawili nchini humo.

Ukraine Kyiv 2026 | Mashambulizi
Shambulizi la Urusi mjini Kyiv nchini Ukraine mnamo Juni 2, 2026Picha: Sergei Supinsky/AFP

Kulingana na chapisho la Huduma ya Dharura ya Ukraine kwenye mtandao wa Telegram hii leo, shambulio hilo la Urusi lilimuua mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 56 aliyekuwa akifanya kazi kama dereva wa basi dogo katika eneo la kusini la Zaporizhzhia.

Katika  shambulio tofauti katika eneo la kati la Dnipropetrovsk, mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 59 aliuawa wakati droni za Urusi pamoja na mabomu ya angani yalipolenga wilaya mbili. Haya ni kwa mujibu wa mkuu wa utawala wa kijeshi wa eneo hilo, Oleksandr Ganzha.

Hayo yanafanyika wakati Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, anatarajiwa kukutana leo na viongozi wa Ufaransa,Ujerumani na Uingereza kwa mazungumzo kuhusu hatua za baadaye, wakati Urusi ikiendelea kukabiliwa na changamoto za kijeshi katika uvamizi wake dhidi ya Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW