1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la droni lasababisha kifo cha mtu mmoja Ukraine

15 Novemba 2025

Mtu mmoja ameuawa na mwengine kujeruhiwa katika mashambulizi makali ya droni ya Urusi kwenye eneo la Dnipro mashariki mwa Ukraine. Haya ni kwa mujibu wa Gavana wa eneo hilo Vladyslav Hayvanenko.

Ukraine Kamianske | shambulizi la droni la Urusi
Uharibifu uliofanywa na shambulizi la Urusi mjini Kamianske, Ukraine mnamo Novemba 11, 2025Picha: Mykola Synelnykov/REUTERS

Maeneo mbalimbali yaliathirika kwa moto katika mji mkuu wa mkoa wa Dnipro, lakini uharibifu pia uliripotiwa kwenye nyumba za watu binafsi na magari katika miji midogo ya Nikopol, Marhanets, Chervonohryhorivka, Synelnykove, na wilayani Myrove.

Urusi pia iliripoti uharibifu kutokana na mashambulizi ya droni za Ukraine.

Wakati jeshi likiripoti kuwa ni droni 64 pekee zilizodunguliwa kwenye anga ya Urusi, Gavana wa Ryazan, Pavel Malkov, amethibitisha kuwa mabaki ya droni yalioanguka yalisababisha moto kwenye eneo la kampuni moja iliyoripotiwa na tovuti ya Astra kuwa kiwanda cha kusafisha mafuta.

Malkov pia amesema hakukuwa na majeruhi, na kiwango cha uharibifu bado kinafanyiwa tathmini.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW