1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la Israel Beirut laua watu 11

23 Novemba 2024

Mashambulizi ya anga ya Israel katikati mwa jiji la Beirut yamesababisha vifo vya takriban watu 11 na kuporomosha jengo la makazi huku Israel ikiendelea na kampeni yake ya anga dhidi ya Hezbollah.

Libanon Beirut 2024 | Rettungskräfte durchsuchen nach israelischem Luftangriff nach Opfern
Picha: Hassan Ammar/AP Photo/picture alliance

Shambulio hilo lilifuatiwa na mengine katika vitongoji vya kusini mwa mji huo baada ya wito wa jeshi la Israel kuwataka watu kuhama katika eneo hilo. Shughuli za uokoaji zimeripotiwa kuendelea huku waokoaji wakiondoa vifusi vya jengo hilo la ghorofa nane, na gari la zimamoto walinzi wa raia wakiwa katika eneo la tukio. Wizara ya Afya ya Lebanon imesema mbali ya vifo hivyo 11 watu wengine 63 wamejeruhiwa. Rekodi jumla za wizara hiyo zinasema zaidi ya watu 3,645 wameuwawa tangu Oktoba 2023.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW