1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Shambulizi la Israel Gaza lasababisha vifo vya watu 9

20 Aprili 2024

Shirika la ulinzi wa raia wa Gaza limesema leo kuwa shambulizi la usiku kucha la Israel limesababisha vifo vya watu tisa wa familia moja ya Kipalestina katika eneo la Tal-al-Sultan lililoko mji wa kusini wa Rafah

Picha za uharibifu mkubwa uliosababisha na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza
Majengo yalioporomoka kutokana na mashambulizi ya Israel GazaPicha: Ali Jadallah/Anadolu/picture alliance

Kwa mujibu wa hospitali ya Al Najjar, watoto watano wa umri wa kati ya mwaka mmoja na miaka saba pamoja na msichana mwenye umri wa miaka 16, walikuwa miongoni mwa waliouawa. Wanawake wawili na mwanamme mmoja pia walipoteza maisha yao.

Katika taarifa, msemaji wa shirika hilo la ulinzi, Mahmud Bassal, amesema kuwa watu hao aliowaita mashahidi, walifukuliwa kutoka kwa vifusi vya nyumba yao.

Soma pia: Israel yaendelea kuitwanga Gaza, wasiwasi wa vita na Iran wazidi

Bassal amesema jeshi la Israel lilishambulia maeneo kadhaa ya mji huo wa Rafah pamoja na kitongoji cha Salam, ambapo mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Pia ameongeza kuwa jeshi hilo lililenga nyumba na shule moja ya chekechea na kwamba umekuwa usiku wa mahangaiko kwa wakaazi wa eneo hilo.