1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la Israel la leo lauwa watu 18 Gaza

4 Agosti 2024

Mashambulizi ya Israel ya mapema leo yamewauwa watu 18 huko Gaza wakiwemo wanne ambao walikuwa wamejihifadhi katika hema la kambi moja ya wakimbizi iliyo kwenye eneo la hospitali.

Mashambulizi ya Israel katika hospitali ya al-Aqsa Martyrs
Taswira vya eneo lililoharibiwa baada ya shambulio la Israeli huko Deir al-Balah, Gaza Agosti 4, 2024.Picha: Ashraf Amra/picture alliance/Anadolu

Hilo linatokea huku kukiwa na taarifa za Mpalestina kuwauwa watu wawili, mwanamke wa miaka 70 na mwanaume wa miaka 80 kwa kuwashambulia kwa kisu katika viunga vya mji wa Tel Aviv.

Wakati kukiripotiwa matukio hayo ya mauwaji, Wizara ya Afya yaGaza chini ya kundi la Hamas imesema takribani watu 39,583 wameuwawa katika miezi karibu 10 ya vita kati ya Israel na Hamas.

Takwimu hizo zinajumuisha vifo 33 ambavyo vimetokea katika kipindi cha saa 24. Watu 91,398 wamejeruhiwa tangu Hamas ifanye shambulizi la Oktoba 7 huko Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW