Shambulizi la Israel lawauwa watu sita Gaza
14 Machi 2026
Matangazo
Shirika hilo la ulinzi wa kiraia la Gaza, limesema kuwa wakati wa shambulizi hilo lililotokea leo alfajiri, polisi wawili na raia mmoja waliuawa katika mji wa kusini wa Khan Yunis.
Pia limesema kuwa shambulizi la jana jioni dhidi ya kundi la raia mashariki mwa Gaza City lilisababisha vifo vya watu watatu ambao miili yao ilipelekwa katika hospitali kuu ya eneo hilo Al- Shifa.
Hata hivyo jeshi la Israel halikujibu ombi la tamko kuhusu tukio hilo.