1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la kigaidi lauwa watu 20 nchini Somalia

21 Agosti 2022

Watu 20 wameuwawa baada ya kutokea shambulizi la kigaidi katika hoteli moja mjini Mogadishu, nchini Somalia.

Somalia mehrere Tote bei Angriff auf Hotel Hayat in Mogadischu
Picha: Feisal Omar/REUTERS

Kwa mujibu wa polisi pamoja na watu wengine walioushuhudia mkasa huo, kundo la wenye itikadi kali lilishiriki makabliano na vikosi vya usalama kwa masaa kadhaa ambayo yalihitimishwa kwa vifo vya watu 20.

Nyongeza ya hayo, watu wengine 40 wameripotiwa kujeruhiwa kwa mkasda huo uliotokea usiku wa kuamkia Jumamosi. Lakini vikosi vya usalama vilifanikiwa kuwaokoa wengine kadhaa wakiwemo watoto, katika hoteli hiyo maarafu ya mjini Mogadishu ifahamikayo kama "Hayat Hotel."

Polisi imefanikiwa kumuuwa gaidi ya mwisho aliyejificha jengoni

Afisa wa usalama wa Somalia akiwa katika doriaPicha: Feisal Omar/REUTERS

Baada ya washambuliaji kuingia ndani ya hoteli hiyo na kufyatua risasi miripuko miwili ilitokea nje ya hoteli hiyo. Vikosi vya Somalia vimehitimisha operesheni ya kijeshi iliyodumu kwa tajkribani masaa 30 ambayoo imefanikisha kumuua mtu mwenye silaha aliyejificha ndani ya jengo la hoteli.

Vikosi vya ulinzi wa amani wa jumiuiya za kimatiafa ikiwemo ile ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika imelaani vikali shambulizi hilo.

Kundi la Al-Shabaab ladai kuhusika na shambulizi hilo.

Kudi la wenye itikadi kali la al-Shabaab, lenye mfungamano na al-Qaeda limedai kuhusika na shambulizi hilo,  likiwa ni muendelezo wa mengine kadhaa yenye kuyalenga maeneo ambayo yanatembelewa mara nyingi na maafisa wa serikali.

Shambulizi hilo ni kubwa zaidi kutoka nchini Somalia tangu kuingia madarakani kwa kiongozi mpya wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud ambae ameingia madarakani mwezi Mei.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, ubalozi wa Marekani nchini Somalia imelilaani shambulizi katika hoteli ya Hayat. Pamoja na kutoa pole kwa waathirika, ubalozi huo umetoa ahadi ya kuisaidia Somalia kufanikisha walifanya vitendo hivyo wanawajibishwa na kushiriki katika ujenzi katika kipindi hiki ambacho wengine wanabomoa.

Soma zaidi:Rais mpya wa Somalia aapa kukabiliana na ugaidi

Hakuna taaarifa za haraka katika utambuzi wa waliuwawa lakini idadi kubwa inaaminika kuwa ni raia wa kawaida. Hadi wakati huu al-Shabaab inasalia kundi lenye athari kubwa katika eneo la Pembe ya Afrika.

Kundi hilo limedhibiti maeneo mengi katika siku za hivi karibuni, likitumia mwanya msuguano uliopo baina ya vikosi vya usalama vya Somalia pamoja na kutokukubaliana kati ya serikali na majimbo.

Chanzo: AP