1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Kambi ya jeshi yashambuliwa nchini Mali

8 Septemba 2023

Jeshi la Mali limesema kambi yake kaskazini mwa nchi imelengwa katika shambulizi la kujitoa mhanga, siku moja tu baada ya mashambulizi mabaya ya wanamgambo na kuua watu 64.

Mali Unruhen Soldaten
Picha: Sebastien Rieussec/Hans Lucas/IMAGO

Jeshi hilo limesema kupitia mitandao ya kijamii kwamba uwanja wa ndege uliko  mjini Gao  umepigwa katika kile lilichokiita shambulio gumu. Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi, ila tu kwamba majibu na tathmini vinaendelea.

Kanda ya Sahel imeshuhudia kuzuka tena kwa hali ya wasiwasi katika wiki za hivi karibuni, iliyochochewa kwa sehemu na kuondolewa kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Mali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW