1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Shambulizi la Marekani lawauwa wanamgambo wa Al-Shabaab

Daniel Gakuba
17 Februari 2023

Kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika, AFRICOM, imesema Marekani imewauwa wanamgambo watano wa al-Shabaab katika shambulizi lililolenga ngome ya kundi hilo la kigaidi karibu na mji wa Bacadweyne.

Somalia Militants Twitter
Picha: picture alliance / AP Photo

AFROCOM imesema katika tangazo lake kuwa shambulizi hilo lilifanyika Jumatano kufuatia ombi la serikali ya mjini Mogadishu. Viongozi wa Somalia na mataifa jirani walifanya mkutano mapema mwezi huu na kuapa kulipa kipigo cha mwisho kundi la al-Shabaab lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida ambalo limekuwa likiendesha uasi katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kwa zaidi ya miaka 15. Mnamo miezi ya hivi karibuni, jeshi la Somalia na wanamgambo wa kiukoo ambao ni washirika wake limefanikiwa kuyakomboa maeneo makubwa yaliyokuwa chini ya udhibiti wa al-Shabaab. Vikosi vya Umoja wa Afrika na mashambulizi ya anga ya Marekani vimchangia kuipa msukumo serikali ya Mogadishu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW