1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la RSF lauwa watu 8 El-Fasher, Sudan

8 Oktoba 2025

Shambulizi la droni lililofanywa na wanamgambo wa RSF nchini Sudan limewauwa watu wanane katika wodi ya kina mama wajawazito kwenye mji wa El Fasher.

Athari iliyotokana na mashambulizi huko El Fasher
Athari iliyotokana na mashambulizi huko El FasherPicha: AFP

Haya ni kwa mujibu wa chanzo cha kimatibabukilichozungumza na Shirika la Habari la Ufaransa, AFP.

Kulingana na chanzo hicho, shambulizi hilo pia liliwajeruhi watuwengine saba na kuharibu majengo na vifaa. Hospitali hiyo iliyoshambuliwa ni mojawapo ya hospitali zilizosalia zinazofanya kazi katika eneo hilo huku nyingi zikiwa zimeshambuliwa kwa mabomu na kulazimika kufunga milango yake.

Wanaharakati wanasema mji wa El-Fasher umekuwa kama "chumba cha wazi cha kuhifadhia maiti"kwa raia wanaokabiliwa na njaa.

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa zilizotolewa jana, zaidi ya watu milioni moja wameukimbia mji wa El-Fasher tangu kuanza kwa vita, hiyo ikiwa asilimia 10 ya wakimbizi wa ndani nchini humo.