1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la Urusi laua mmoja na kujeruhi watu 46 Ukraine

2 Novemba 2024

Maafisa wa huduma za dharura nchini Ukraine wamesema mtu mmoja ameuawa na watu wengine 46 wamejeruhiwa katika shambulio la kombora la Urusi katika kituo cha polisi katika mji wa mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv.

Ukraine
Polisi wa Ukraine ni miongoni mwa waliojeruhiwa katika shambulizi la UrusiPicha: George Ivanchenko/Anadolu/picture alliance

Maafisa wa huduma za dharura nchini Ukraine wamesema mtu mmoja ameuawa na watu wengine 46 wamejeruhiwa katika shambulio la kombora la Urusi katika kituo cha polisi katika mji wa mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv siku ya Jumamosi.

Kituo hicho cha polisi inaaminika kuwa kilishambuliwa mara mbili kwa makombora hapo jana ambapo taarifa za awali zilisema karibu watu 30 walijeruhiwa.

Soma zaidiZelenskiy: Mataifa ya magharibi mnapaswa kutusaidia zaidi

Lakini kufikihii leo idadi ya waliojeruhiwa imepanda huku maafisa wa polisi 36 wakiwa ni miongoni wa waliojeruhiwa katika shambulio hilo la Urusi.

Mashambulizi hayo yanaendelea kufanyika wakati rais wa Ukraine, Volodymyir Zelenskiy akiwatolea mwito washirika wake wa magharibi kuchukua hatua kuisaidia nchi yake na kuacha kulinyamazia suala la uwepo wa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW