SiasaUkraine
Watu 51 wauawa kwenye shambulizi mjini Kharkiv
6 Oktoba 2023Matangazo
Shambulio hilo lililoibua hasira kutoka kwa viongozi wa nchi za Magharibi, lililenga mkusanyiko watu waliokuwa msibani katika kijiji cha Groza.
Msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa eneo hilo Dmytro Tchoubenko, amesema msiba huo ulikuwa wa mwanajeshi wa Ukraine aliyekufa katika mapigano, ambaye pia mkewe na mwanawe waliuawa katika shambulio hilo. Viongozi mbalimbali wa Magharibi wamelaani shambulio hilo.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye kwa sasa yupo nchini Uhispania kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Ulaya, amelaani shambulio hilo na kulitaja kuwa la kigaidi huku akiwatolea wito viongozi wa Umoja wa Ulaya kuipatia nchi yake mifumo zaidi ya ulinzi wa anga.