1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Shambulizi ya kujitoa muhanga laua watu 6 Afghanistan

27 Machi 2023

Mamlaka nchini Afghanistan zimesema kuwa raia 6 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kufuatia shambulizi la kujitoa muhanga hii leo karibu na wizara ya mambo ya nje mjini Kabul.

Afghanistan | Explosion vor Außenministerium in Kabul
Picha: Wakil Kohsar/AFP/Getty Images

Hilo ni shambulio la pili karibu na wizara hiyo kwa muda usiozidi miezi 3.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan, Abdul Nafy Takor, amesema mshambuliaji alipigwa risasi na vikosi vya usalama lakini hilo halikuzuia mabomu aliyokuwa nayo kuripuka. Hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo.

Licha ya kuwa usalama umeimarika tangu kundi la Taliban kurejea madarakani Agosti mwaka 2021, na kuiondoa serikali inayoungwa mkono na Marekani na kumaliza uasi wao wa miongo miwili, lakini kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu, IS, limeonekana kuwa tishio.