1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiChina

Shanghai yakabiliwa na ongezeko la maambukizi ya Corona

22 Desemba 2022

Maambukizi ya virusi vya Corona yanaongezeka katika mji wa kibiashara wa Shanghai huko China ambapo hospitali ya mji huo imewaambia wafanyakazi wake kujiandaa kwa mapambano makubwa.

China | Corona Proteste | Polizeipräsenz in Shanghai
Picha: Hector Retamal/AFP/Getty Images

Hospitali hiyo imeeleza kwamba inatarajia nusu ya wakaazi milioni 25 wa mji huo kuambukizwa kufikia mwishoni mwa mwaka wakati virusi hivyo vikienea China bila ya kugundulika.

Baada ya maandamano na visa vya maambukizi kuongezeka, China mwezi huu iliamua kubadili ghafla sera zake na kuanza kuondowa vizuizi vya kupambana na Uviko-19, ambavyo vilisababisha wakaazi wa taifa hilo kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi na kisaikolojia.

Hospitali hiyo ya Shanghai, Deji imechapisha kwenye ukurasa wake rasmi katika mtandao wa kijamii wa We Chat taarifa ikisema watu wanaokadiriwa kufikia milioni 5.43 wameambukizwa katika mji huo na wengine milioni 12.5 wataambukizwa kufikia mwishoni mwa mwaka.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW