1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHARM EL SHEIKH:Iran yaishambulia Marekani na kusema isimtafute mchawi wa matatizo ya Iraq

4 Mei 2007

Iran imetupa makombora makali dhidi ya siasa za Marekani nchini Iraq na kusema kuwa kuwepo kwake huko ndiko chanzo cha umwagikaji mkubwa wa damu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Manouchehr Moattaki akizungumza katika mkutano wa kimataifa juu ya Irak nchini Misri amesema Marekani ni lazima ikubali kuwa kuongezeka kwa maasi nchini Iraq, ni kutokana na kuwepo kwao huko na wasitafute mchawi.

Mapema ilielezwa kuwa Waziri huyo wa nje wa Iran ilikuwa akutane hii leo pembezoni mwa mkutano huo, na waziri wa nje wa Marekani Condoleza Rice.Hata hivyo bi Rice amesema kuwa bado hawajatana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW