SHARM EL SHEIKH:Ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani nchini Misri
20 Juni 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani bi Condoleeza yupo ziarani nchini Misri. Kwenye ziara hiyo bibi Rice amefanya mazungumzo na rais wa Misri Hosni Mubarak na waziri mkuu wa Misri Ahmed Aboul Gheit.
Bibi Rice ameitolea wito serikali ya Misri kufanya uchaguzi huru na wa haki.
Ziara hiyo inalenga kuhimiza mabadiliko ya kidemokrasi kwenye eneo hilo.
Hapo jana waziri Rice aliipongeza Israel kwa kupiga hatua juu ya suala la mpango wa amani lakini, hata hivyo muda mfupi baada ya mkutano wake na waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon mjini Jerusalem,Wizara ya Ujenzi ya Israel ilitoa mpango wa kujengwa makazi 700 mapya katika eneo la magharibi mwa ukanda wa Gaza.
Marekani imeukosoa mpango huo wa Israel.