1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Shehbaz Sharif atarajiwa kuwa waziri mkuu wa Pakistan

14 Februari 2024

Shehbaz Sharif anatarajiwa kuanza muhula wa pili kama waziri mkuu wa Pakistan katika siku zijazo. Kiongozi huyo atarejea wadhfa huo aliokuwa nao kabla ya bunge kuahirishwa kabla ya uchaguzi wa wiki iliyopita.

Pakistan, Lahore | Shehbaz Sharif
Waziri Mkuu wa zamani Pakistan Shehbaz SharifPicha: K.M. Chaudary/AP/picture alliance

Sharif, mwenye umri wa miaka 72, amependekezwa na chama chake cha PML-N na vyama washirika vitakavyounda serikali ya mseto kuliongoza taifa hilo lenye silaha za nyuklia.

Baada ya kuapishwa,Shehbaz Sharifatahitaji kwa mara nyingine tena kuomba mkopo kutoka kwa shirika la fedha la kimataifa IMF huku muda wa mkataba wa mkopo wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwezi ujao.

soma pia:Vyama vya kisiasa Pakistan vyaunda serikali ya muungano

Pakistan inahitaji kuongezewa muda wa kulipa deni lake. Pakistan inaendelea kugubikwa na mzozo wa kiuchumi huku mfumuko wa bei ukisalia kuwa juu, karibu kwa asilimia 30 na wakati huo huo ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo umepungua na kufikia karibu asilimia 2.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW