1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Shehena ya kwanza ya misaada kuelekea Gaza yapakuliwa

16 Machi 2024

Shirika la hisani la Marekani "World Central Kitchen" limesema leo kuwa timu yake imemaliza kupakua shehena ya kwanza ya misaada iliyosafirishwa kwa njia ya bahari kuelekea katika ukanda wa Gaza.

Shehena ya misaada ikipakuliwa kwa ajili ya kusambazwa kwa wakaazi wa Gaza
Shehena ya misaada ikipakuliwa kwa ajili ya kusambazwa kwa wakaazi wa GazaPicha: WORLD CENTRAL KITCHEN via REUTERS

Kupitia taarifa, shirika hilo limeeleza kuwa shehena hiyo ya misaada yenye takriban tani 200 za chakula imeshushwa na iko tayari kusambazwa.

"World Central Kitchen" imelazimika kujenga gati kusini magharibi mwa Gaza ili kusaidia kupakua na kuisambaza misaada hiyo.

Shirika hilo la hisani la Marekani linaanda safari ya mashua ya pili yenye msaada mwengine wa karibu tani 240 za chakula kutokea Cyprus, kituo cha kwanza cha njia mpya ya bahari ya kupeleka misaada Mediterania ya mashariki.

Soma pia: Meli ya misaada kutoka Cyprus taratibu yakaribia Gaza 

Misaada hiyo inajumuisha vyakula vya mkebe ikiwa ni pamoja na bidhaa nyengine kama vile maharagwe, karoti, samaki aina ya jodari, mbaazi, mahindi, mchele, mafuta na chumvi.

Jeshi la Israel limethibitisha kuwa, meli ya kwanza inayoendeshwa na shirika la misaada la Uhispania la Open Arms, pia imewasili na kwamba wanajeshi wake wametumwa katika bandari ili kushika doria na kufanya ukaguzi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW