1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 10 Jela kwa Sheikh Hasina kwa makosa ya ufisadi

2 Februari 2026

Mahakama ya Bangladesh imemhukumu Waziri Mkuu wa zamani Sheikh Hasina, miaka 10 Jela kwa makosa ya ufisadi. Uamuzi huo umetokea wakati serikali ya mpito ikijitayarisha kwa uchaguzi unaoatarajiwa kufanyika Februari 12.

Frankreich Paris 2021 | Sheikh Hasina
Waziri Mkuu wa zamani wa Bangladesh Sheikh Hasina ahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa makosa ya ufisadiPicha: Christophe Ena/AP Photo/picture alliance

Mpwa wa Sheikh Hasina Tulip Siddiq ambaye ni mbunge nchini Uingereza alihuhukumiwa pia kifungo cha miaka 4 jela, katika kesi mbili walizokabiliwa nazo zinazohusiana na Ufisadi.

Jaji Mohammed Rabiul Alam pia alitoa hukumu nyengine ya miaka 7 kwa watu wengine wawili wa familia ya Sheikh Hasina, Azmina Siddiq an Radwan Mujib Siddiq kwa makosa sawa na hayo.

Taasisi ya kupambana na rushwa ya Bangladesh ilianzisha kesi mahakamani dhidi ya waziri Mkuu huyo wa zamani, ikidai alishirikiana na maafisa wa serikali ili kujipatia yeye na familia yake ploti sita katika mpango wa serikali wa Purbachal karibu na mji mkuu Dhaka licha ya kanuni za serikali kumbana kufanya hivyo. 

Uamuzi huo umetokea wakati serikali ya mpito inayoongozwa na aliyewahi kushinda Tuzo ya amani ya Nobel Muhammad Yunus, ikijitayarisha kwa uchaguzi  unaoatarajiwa kufanyika Februari 12. Chama cha Hasina cha zamani cha Awami kimepigwa marufuku kushiriki.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW