Shelly-Ann Fraser-Pryce achukua dhahabu ya mita 100
25 Agosti 2015Matangazo
Ilikuwa ni dhahabu ya sita kwa mwanariadha huyo kushinda baada ya kushinda mbio za mita 100 na 200 mwaka 2013.
Schippers ni bingwa wa mbio za Heptathlon baada ya kushinda medali ya shaba miaka miwili iliopita.
Ni rekodi ya taifa kwa upande wa Schippers ambaye alianza kushiriki katika mbio fupi mnamo mwezi Juni huku Bowie mwenye umri wa miaka 24 akinyakua taji lake kuu la kwanza.
Mwanariadha wa Nigeria aliyepigiwa upatu kufanya vizuri Blessing Ogakbare alishika mkia katika mbio hizo.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo