1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machado kupokelewa tuzo ya amani ya Nobel na mwanawe

10 Desemba 2025

Mshindi wa tuzo ya mwaka 2025 ya Nobel Maria Corina Machado hatoshiriki sherehe ya kukabidhiwa tuzo ya amani ya Nobel mjini Oslo, nchini Norway. Alishinda tuzo hiyo kutokana na kupigania demokrasia Venezuela

Maria Corina Machado na mke wa kiongozi wa upinzani Lilian Tintori wakiwa katika moja ya maandamano ya kupinga kufungwa jela kwa Leopoldo Lopez
Maria Corina Machado na mke wa kiongozi wa upinzani Lilian Tintori wakiwa Caracas, katika moja ya maandamano ya kupinga kufungwa jela kwa Leopoldo Lopez Picha: Leo Ramirez/AFP/Getty Images

Mkuu wa taasisi ya Nobel Kristian Berg Harpviken amesema mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Mvenezuela Corina Machado hatoshiriki sherehe ya kukabidhiwa tuzo hiyo inayofanyika leo mjini Oslo.

Kiongozi wa upinzani wa Venezuela bibi Maria Corina Machado aliyetunukiwa tuzo ya mwaka huu ya amani ya Nobel hatofika Oslo kupokea tuzo hiyo na badala yake atapokelewa tuzo hiyo na binti yake, huku taasisi ya tuzo hiyo maarufu duniani ikishindwa kutoa  tamko mara moja kueleza ni kwanini mwanasiasa huyo hatoshiriki sherehe hizo za kukabidhi tuzo.

María Corina Machado Picha: Jimmy Villalta/Europa Press/IMAGO

Ripoti zinaonesha kwamba mwanasiasa huyo wa Venezuela alionekana mara ya mwisho hadharani miezi 11 iliyopita, huku ikifahamika kwamba alikimbilia mafichoni na hakuwahi kuoneakana tena hadharani tangu Januari 9 wakati alipokamatwa kwa muda mfupi baada ya kujiunga na maandamano ya wanaomuunga mkono mjini Caracas.Venezuela yafunga ubalozi wake Norway baada ya Machado kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel

Upinzani dhidi ya tuzo ya amani ya Nobel 

Wakati sherehe  za kukabidhi tuzo ya Nobel zikifanyika hivi leo Jumatano 10.12.2025 , yameonekana maandamano makubwa mjini Oslo jana jioni nje ya taasisi ya Nobel ambako wanaharakati wa mashirika mbali mbali walikusanyika kuipinga tuzo ya amani ya Nobel wanayosema inahalalisha uingiliaji kati kijeshi wa rais Trump katika mataifa mengine.Lina Alvarez Reyes  ni mshauri wa masuala ya habari katika kamati ya mshikamano ya Norway kwaajili ya kanda ya Amerika Kusini.

''Tunaandamana hapa hivi leo kwasababu tunapinga vitisho vya Trump na jeshi la Marekani na uingiliaji kati wa kijeshi katika mataifa ya Venezuela na kanda ya Amerika ya Kusini. Kadhalika tuko hapa kupinga namna tuzo hiyo ya amani hivi sasa inavyotumika kuhalalisha Uingiliaji kati kijeshi wa Marekani katika kanda hiyo'' 

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela akizungumza akiwa kwenye hafla moja ya kiserikali saa chache kabla ya sherehe za kukabidhi tuzo ya Nobel hivi leo, ameyapongeza maandamano yaliyofanyika Oslo akiyaita ni sauti ya kupinga vita. Wakati mpinzani wa rais Maduro, Maria Machado akipongezwa na wengi kwa juhudi zake za kutaka kuleta demokrasia nchini Venezuela,anakosolewa pia na wengine kwa kujiegemeza upande wa rais Donald Trump.

Mwenyekiti wa kamati ya Nobel Joergen Watne Frydnes, Picha: Rodrigo Freitas/NTB/IMAGO

Bibi Machado alikwenda umbali hadi wa kusema anamtunuku tuzo hiyo rais Trump.Jinsi Tuzo ya Amani ya Nobel inavyoamuliwa - siri za mchakato

Rais Trump anayemuunga mkono Machado amekuwa akisema waziwazi kwamba siku za Maduro madarakani zinahesabika.

Sherehe ya kukabidhi tuzo ya Nobel kwa washindi wa vitengo vingine inafanyika Stolkholm Sweden.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW