1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sherehe za 173 za biya mjini Munich

15 Septemba 2006

Shwerehe za biya-Oktoberfest zinafunguliwa leo hii mjini Munich

Picha: AP

Katika jimbo la kusini mwa Ujerumani la Bavaria, homa ya siku kuu ya October imeshaanza kupanda.Saa sita juu ya alama mchana huu wa leo,diwani wa jiji la Munich Christian Ude atafungulia mfereji wa pipa la kwanza la biya kwa sauti kali “O’ zapft is”.Kuanzia hapo wageni zaidi ya milioni sita kutoka kila pembe ya dunia wataanza kujistarehesha kwa biya na ngoma za kienyeji katika sherehe hizi za jadi mashuhuri kabisa ulimwenguni.

Kwa muda wa wiki mbili nzima,hadi October tatu, wageni zaidi ya milioni mbili na wenyeji wa jimbo hilo la kusini la Bavaria wanaovalia mavazi yao ya kupendeza ya kiasili watasherehekea siku kuu ya 173 ya October-kama wenyewe wanavyoiita “Oktoberfest”,pakiwepo sherehe mbali mbali na ngoma za kienyeji.Waandalizi wa shamra shamra hizo wameshatayarisha maapipa yasiyohesabika ya biya kwaajili hiyo.

Sherehe hizo kama ilivyo kawaida zitafunguliwa na diwani wa jiji la Munich, safari hii ni Christian Ude wa kutoka chama cha Social Demnocratic kwa kufungua pipa la mwanzo la biya,saa sita juu ya alama kwa saa za ulaya ya kati.

Mwaka jana palihitajika zaidi ya hekotolita milioni sita la laki moja za biya kwa wageni milioni sita na safari hii,kiwango hicho kitapindukia,bila ya kutaja matani kadhaa ya nyama ya soseji na mapande mengine ya nyama ya nguruwe.Lakini hata kuku wa kuchoma na mikate mikavu inayomwagiwa chunvi mashuhuhuri kwa jina la Brezel,na vitamtam vyenginevyo vinapatikana katika sherehe hizi za Oktober fest.

Waandalizi wa shamra shamra hizi wametenga kwa mara ya kwanza safari hii eneo marufuku kwa sigara kati ya maeneo 75 (mahema,mikahawa na mahala pa nyama choma) yaliyotawanyika katika uwanja wa Theresienwiese –bustani ya hekari 31 magharibi ya Munich.

Chengine kipya katika sherehe za mwaka huu za Oktober ni kutengwa eneo kubwa kabisa katika bustani ya Theresienwiese kwaajili ya watoto.

Na muziki nao hautapindukia vipimo vya decibel 85 ili kuweza kuwavutia familia na watu wazee.

Safari hii pia biya itamiminika kwa siku 18 mfululizo badala ya siku 16 za kawaida-kwasababu waa ndalizi wameamua kurefusha hadi jumanne october tatu-ambayo ni siku ya muungano wa Ujerumani,badala ya jumapili october mosi.

Mwanasaikolojia wa mjini München aliyeandika kitabu kuhusu sherehe za Oktober,bibi Brigitt Veiz anasema:

„Kila kitu kinaruhusiwa katika kipindi kizima cha siku 16 kuliko hali inavyokua kawaida.Jazba zinapanda na kila mmoja anajihisi mwepesi na huru kusema au kutenda akitakacho.Mtu anahisi anaweza kupiga makelele,anaruhusiwa kuimba kwa sauti ya juu,kupiga mayowe,kushangiria na hata kuropokwa-kunywa mpaka ukachoka,kumwaga biya ovyo ovyo,na hata kutapika ,kulala na kufanya mapenzi hadharani.“

Sherehe za oktober zimeanzishwa mwaka 1810 wakati wa harusi ya mwanamfalme wa Bavaria Ludwig na binti mfalme Therese wa Sachsen-Hildburghaus.

´Sherehe za Oktober za mjini Munich zimeshaanza kuigizwa kwengineko ulimwenguni.Kuna aina elfu mbili za sherehe kama hizo za biya hivi sasa kote ulimwenguni,ikiwa ni pamoja na brazil na Canada.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW