Sherehe za kuporomoka ukuta wa Berlin
10 Novemba 2009Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo takriban yote yametuwama juu ya sherehe za jana za kutimu mwaka wa 20 tangu kuporomoka kwa ukuta wa Berlin.Gazeti la NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG laandika:
"Sherehe kubwa za kuadhimisha mwaka wa 20 wa kuporomoka ukuta zililingana kabisa na umuhimu wa kihistoria wa tukeo lenyewe.Kwani, kwa kufunguliwa mipaka 1989 kuliitikiwa kwa namna mbili tu: Furaha ilioje na shukurani nyingi.Kwani, tangu enzi hiyo,Ujerumani imebadilika vizuri.Ungeweza hata kuzungumzia kilichotokea ni maajabu ya kisiasa.
Kwani, nani alieota ndoti kuwa katika enzi ya Ujerumani Mashariki (GDR),kwamba 2009 mwanamke kutoka mashariki mwa ujerumani atakuwa Kanzela wa Ujerumani nzima isiogawika ?
Leo hii hali hiyo ni kawaida.Maisha ya Bibi Angela Merkel yanaonesha katika swali la muungano wa Ujerumani , mafanikio makubwa bila kujali unakubaliana nae katika kila siasa yake."
Gazeti la Ludwigsburger Kreiszeitung linasema kwamba, waliosherehekea jana Novemba 9 ,1989, walikuwa wale ambao hawakuweza kujua vipi hali halisi ilvyokua Ujerumani ilipogawanywa mapande 2 .Sasa, wana wasi wasi wa pamoja kupata kazi, wanagombana nani kutoka kwa nani amepata nini. Wanakumbuka ya zamani na wamebakia na baadhi ya dhana mbuvu juu ya mwenziwe.......Katika hisia zao, wamekumbana na shaka shaka na wakitaka kujiunga na dunia ya utandawazi ambayo ilielekeza katika ........mpango wa pamoja wa Umoja wa ulaya.Gazeti lauliza:
"Hali hiyo inaonekana vipi katika maisha ya kila siku ?Wale raia wa Ujerumani Mashariki (GDR) waliopigania kwa dhati uhuru wao ,yamkini wakijiuliza hivyo.Na ingawa jibu lake hawakulijua, walikua na ujasiri kuona yanatokea mabadiliko kuliko kubakia na hofu.Walipiga mfano mwema."
Ama gazeti la "DER NEUE TAG" laandika kuwa, binaadamu wana desturi ya kuvuka mpaka, ni kawaida.Hatahivyo, kufanya sherehe ndogo tu jana, pia ingetosha.
Gazeti laongeza:
"Haikutosha kukigeuza kisa hicho kuwa show ya Las-Vegas .Kuwaalika wanasiasa wa hadhi ya juu kuwaonesha jinsi gani ukuta ulianguka kwa amani,ingeweza kuepushwa."
Gazeti la NORDBAYERISCHER KURIER laandika kuwa, mwanadamu amebakia kuwa mfungwa katika mipaka anamoishi hata ikiwa ana uhuru wa kwenda.Furaha ya muda mfupi haukupita muda, iligubikwa na ukweli wa maisha ya kawaida,
Gazeti laongeza:
"Si watu wachache miaka 20 iliopita, waliotazamia kuingia ulimwengu mpya na wa maisha bora.Mpambano mkubwa wa kijeshi uliepukwa,majeshi yakatoweka na silaha zikakongolewa. Lakini, tangu enzi hizo, kumezuka vita vingi vidogo-vidogo ambavyo vilipalilia uwezekano wa kuzuka vita vikubwa.Nini la kufanya kwa maarifa kama hayo miaka 20 baada ya mabadiliko hayo ya matumaini makuu ?"
Ama gazeti la Kölnische Rundschau, linakueleza kuanguka ukuta, hakujakuwa kazi rahisi:Ilikua kazi ngumu,ya mtafaruku,ya bahati na kubabaisha-chanzo chake ni kikubwa .Na jinsi matokeo yake hayana mpaka, maadhimisho ya mwaka wa 20 yalikuwa mtihani mkubwa kuamua vipi kuadhimisha ukumbusho huo wa hatima ya Ujerumani. Kölnische Rundschau likamaliza:
"Ni jambo zuri kuona Berlin jana ilisherehekea, tena kwa shangwe na shamra shamra na hiyo ndio njia pekee iliofaa, kukumbuka kuporomoka ukuta."
Mtayarishaji: RamadhanAli /DPA
Mhariri:Abdul-Rahman