Sherehe za miaka 100 ya Jengo la Bauhaus Dessau-Roßlau
24 Februari 2019Maadhimisho ya miaka mia moja tangu jengo hilo la kale lilipojengwa yameanza Dessau, chini ya kauli mbiu" limekomaa kuwa Makumbusho?". Sherehe zilizoanza jana za jengo hilo lililofanyiwa ukarabati ni mwanzo tu wa kile kitakacho shuhudiwa sherehe zenyewe hasa zitakapofanyika. Jengo jipya ambalo ufunguzi wake rasmi , septemba nane inayokuja ndio utakaokuwa kilele cha sherehe jumla mwaka huu, linawafungulia milango kwa mara ya kwanza watu wa kawaida kulitembelea. Msemaji wa wakfu wa Bauhaus katika mji wa Dessau amesema wanataraji watu zaidi ya 1500 watalitembelea jengo hilo .
Mikururo wanasubiri kuingia ndani ya jengo hilo
Milolongo ya watu wamepiga foleni hata kabla ya jengo hilo kufunguliwa, kwakuwa kawaida watu 400 tu ndio wanaoruhusiwa kuingia kwa wakati mmoja."Wamejaa kweli kweli" amesema mkurugenzi wa wakfu huo Claudia Perren akifurahia jinsi umati wa watu wanavyoonyesha shauku na kuvutiwa na sherehe za miaka 100 ya ujenzi wa Bauhaus.
Hafla hiyo ya siku moja ni mwanzo tu wa ratiba jumla ya sherehe za miaka mia moja za jengo la Bauhaus katika mji wa Dessau-Roßlau. Ratiba hiyo inajumuisha burudani za muziki, maonyesho, majadiliano ya wataalam kuhusu mradi wa Bauhaus, warsha na mengineyo. Zaidi ya hayo wanaotembelea jengo hilo watajionea progamu tofauti mjini Dessau. Ratiba ya sherehe za miaka miaka moja za Bauhaus itafafanuliwa na mkurugenzi wa wakfu wa Bauhaus Claudia Perren. Zaidi ya hayo waziri wa utamaduni wa jimbo la Saxon-Anhalt Rainer Robra wa chama cha CDU amepangiwa kuwalahiki watakaoliteembelea jengo hilo.
Bauhaus limetangazwa kuwa turathi za kimataifa na shirika la kimataifa la UNESCO
Jengo la Bauhaus limejengwa mwaka 1919 huko Weimar na msanifu majengo Walter Gropius aliyeishi kati ya mwaka 1883 hadi mwaka 1969. Baadae shule ya Bauhaus ikahamishiwa Dessau na kufunguliwa Berlin kabla ya kufungwa kutokana na shinikizo la utawala wa wanazi mwaka 1933. Hadi wakati huu jengo la Bauhaus linasifiwa ulimwenguni kutokana na mtindo wa ujenzi wa kuvutia, sanaa na usanifu muundo. Mjini Dessau jengo la Bauhaus limeshuhudia enzi zake za fahari kama shule kati ya mwaka 1925 hadi 1932. Majengo ya Bauhaus mijini Waimar na Dessau-Roßlau sawa na Bernau katika jimbo la Brandenburg yametangazwa na shirika la Umoja wa mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO kuwa turathi za kimataifa.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/epd
Mhariri: Sylvia Mwehozi