Baada ya kipindi kirefu cha mauaji ya zaidi wapigania demokrasia 30 nchini Iraq, hatimaye mmoja wa washukiwa ametiwa mbaroni. Lakini pamoja na hatua hiyo bado maelfu ya wanaharakati wameendelea kuishi kwa wasiwasi.
Matangazo
Kwa miezi kadhaa sasanchini Iraq, wanaharakati, wachambuzi na waandishi wa habari, kwa ujumla yeyote ambae amekuwa akizungumza waziwazi kupigia chapuo mabadiliko ya kisiasa nchini humo anakuwa katika hali ya hatari.
Kwa mujibu wa rekodi za asasi za kupigania haki za binaadamu katika kipindi cha miezi 18 kumekuwepo na vifo vya zaidi ya wanaharakati 35 na majaribio ya mauaji 18. Hayo yametokea tangu kuanza kwa vuguvugu la maandamano maarufu, 2019 ambalo lililazimisha mabadiliko ya kiuongozi.
Serikali ya Iraq imetoa ahadi ya kuvifanyia uchunguzi vitendo vya mauwaji, lakini hadi sasa hakuna chochote kilichofanyika. Miongoni mwa waliokufa wamo wanaharakati maarufu kama Ihab al-Wazni, ambae alikuwa akiratibu maandamano katika mji wa kusini mwa Iraq wa Karbala.
Aliuwawa kwa kupigwa risasi mwanzoni mwa mwezi uliopita. Mwezi Juni mwaka jana aliuwawa mchambizi maarufu wa masuala ya usalama Hisham al-Hashimi, katika tukio ambalo liligonga vichwa vya habari vya ulimwengu.
Wanaharakati wengine maarufu, kama Ali Jasb Hattab Aboud, ambae ni mwanasheria mbobezi katika masuala ya haki za binaadamu, ambae alikuwa akitoa usaidizi wa kisheria kwa waandamanaji, ametekwa nyara na hajaweza kuonekana tena hadi leo. Katika jambo linalosikitisha zaidi miongoni mwa waliuwawa yumo baba wa Aboud, ambae alikuwa akipigania haki ya mwanawe katika mahakama ya Iraq. Aliuwawa kwa kupigwa risasi Machi 2020.
Baadhi ya mauwaji, kama ya al-Hashimi, al-Wazni na Aboud baba yaliweza kunaswa kupitia kamera za usalama. Na vidio zimeonesha kwa kiwango fulani cha kufanana kwa namna gani wauwaji walivyokuwa wakiwasili katika maeneo ya tukio, wakiwa na gari au pikipiki. Wengi waliouwawa ni wakosoaji kwa kuhusishwa tu na hujuma ya kikosi maalumu cha ulinzi nchini Iraq kinachojulikana kama PMF.
Mzozo wa kudumu — Miaka 40 tangu kuanza kwa vita vya Iran-Iraq
Vita vya Iran-Iraq ni mmoja ya mizozo mibaya zaidi ya kijesi ya Mashariki ya Kati. Mzozo huo uliodumu kwa miaka 8, ambamo silaha za kemikali zilitumiwa, uliua maelfu ya watu na kuigawa kanda kwa misingi ya madhehebu.
Picha: picture-alliance/Bildarchiv
Mabishano ya ardhi
Septemba 22, 1980, kiongozi wa Iraq Saddam Hussein alituma majeshi katika nchi jirani ya Iran, na kuanzisha vita mbaya iliyodumu kwa miaka minane ambamo maelfu ya watu waliuawa. Vita hiyo ilianzia kwenye mzozo juu ya ardhi kati ya mataifa hayo mawili yenye waumini wengi wa Kishia.
Picha: defapress
Mapatano ya Algiers
Miaka mitano kabla, mnamo Machi 1975, Hussein, wakati huo makamu wa rais wa Iraq, na Shah wa Iran walisaini makubaliano mjini Algiers kutatua mzozo wa mpakani. Baghdad hata hivyo, iliituhumu Tehran kwa kupanga njama ya mashambulizi na ikatoa wito wa kuondolewa watu kwenye visiwa viwili vya kimkakati katika njia ya bahari ya Hormuz, vilivyodaiwa na mataifa yote mawili pamoja na UAE.
Picha: Gemeinfrei
Chanzo muhimu cha maji
Septemba 17, 1980, Baghdad iliyatangaza makubaliano ya Algiers kuwa batili na ikadai udhibiti wa Shatt al-Arab yote - mto wenye urefu wa kilomita 200 unaotengenezwa kwa kukutana Tigris na Euphrates, ambayo inatiririka kwenye ghuba.
Picha: picture-alliance/AP Photo/N. al-Jurani
Mashambulizi ya bandari na miji
Vikosi vya Hussein vilishambulia viwanja vya ndege vya Iran kwa mabomu, kikiwemo cha Tehran, pamoja na miundombinu ya kijeshi na mitambo ya mafuta. Vikosi vya Iraq vilikumbana na upinzani mdogo katika wiki ya kwanza na viliteka miji ya Qasr-e Shirin na Mehran, pamoja na bandari ya kusini-magharibi mwa Iran ya Khorramshahr, ambako mto Shatt al-Arab unakutana na bahari.
Picha: picture-alliance/Bildarchiv
Adui wa pamoja
Mataifa mengi ya Kiarabu, zikiwemo Saudi Arabia na Kuwait, yaliiunga mkono Baghdad katika vita dhidi ya Iran, yakihofia kwamba mapinduzi ya Kiislamu yalioongozwa na Ayatollah Khomeini yangeweza kuwashawishi waumini wa Kishia katika Mashariki ya Kati. Mataifa ya Magharibi pia, yaliisaidia Baghdad na kuuza silaha kwa utawala wa Hussein.
Picha: Getty Images/Keystone
Iran yajibu mashambulizi
Mashambulizi ya kujibu ya Iran yaliishtua Iraq, baada ya Tehran kufanikiwa kurejesha udhibiti wa bandari ya Khorrramshahr. Baghdad ilitangaza kusitisha mapigano na kuondoa vikosi vyake, lakini Tehran ilikataa mpango huo na kuendelea kuishambulia miji ya Iraq. Kuanzia Aprili 1984, pande mbili zilishiriki "vita vya miji", ambamo miji ipatayo 30 kwa kila upande ilishambuliwa kwa makombora ya masafa.
Picha: picture-alliance/dpa/UPI
Silaha za kemikali
Moja ya matukio makuu ya vita vya Iran-Iraq lilikuwa matumizi ya Baghdad ya silaha za kemikali dhidi ya Iran. Tehran ilianza kutoa madai hayo 1984 - na kuthibitishwa na UN - na kisha tena mnamo 1988. Juni 1987, vikosi vya Iraq vilidondosha mabomu ya gesi katika mji wa Iran wa Sarasht. Machi 1988, Iran ilidai kwamba Baghdad ilitumia silaha za kemikali dhidi ya raia wa Iraq katika mji wa Halabja.
Picha: Fred Ernst/AP/picture-alliance
Mapatano
Julai 18, 1988, Khomeini alikubali azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kumaliza vita. Wakati idadi halisi ya waliouawa katika vita hiyo haijulikani, watu wasiopungua 650,000 walikufa wakati wa mzozo huo. Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitangazwa Agosti 20, 1988.
Picha: Sassan Moayedi
Ukurasa mpya
Kuondolewa kwa utawala wa Hussein na Marekani mwaka 2003, kulianzisha zama mpya katika Mashariki ya Kati. Uhusiano kati ya Iraq na Iran umeboreka tangu wakati huo, na mataifa hayo mawili yanazidi kushirikiana katika nyanja za kiuhumi, kitamaduni na kijamii.
Kikosi hicho PMF, ambacho kiliundwa mahususi kwa ajili ya kukabiliana na kundi la Dola la Kiislamu ambapo pamoja na adui yao mkubwa kuangamizwa kwa kiasi kikubwa, idadi kubwa ya wapiganaji wa PMF bado wanaendeleza utiifu kwa Iran. Iran ndiyo iliyokuwa ikitoa msaada wa vifaa, mafunzo ya kijeshi na fedha wakati wa makabiliano yake na kundi la Dola la Kiislamu.
PMF yashukiwa kuhusika na mauaji
Inaaminika kwamba utekaji nyara na mauwaji vinafanywa na PMF au kikundi kipya cha kuteleza harakati hizo. Wanaharakati wamekuwa wakizitoa tuhuma hizo waziwazi kabisa, jambo ambalo wanasema limekuwa likisababishwa waishi katika vitisho kila siku.
Wawili miongoni mwao wameliambia shirika la habari la DW, kwamba wengi miongoni mwao wanaishi kwa kificho. Mmoja miongoni mwa hao amenukuliwa akisema "Kuna kampeni ya nguvu ya kutaka niuwawae, na najua nipo hatarini" Bwana huyo alizungumza kwa masharti ya kutolitaja jina lake.
Kwa pamoja walisema wamezifunga kurasa zao za mitandao ya kijamii na kubadili akauti zao za barua pepe pamoja na nambari za simu. Wanasema baadhi yao wanabadili maeneo ya kulala kila usiku, kuhama kutoka nyumba moja kwenda nyingine. Huku wengine wanajaribu kuondoka katika nchini humo.
Iraq kwatibuka tena
01:08
Wanahakati wameiambia DW kwamba wana imani kuwa maelfu ya watu miongoni mwao wamekimbia nchini Iraq kutokana na uwepo wa kampeni ya kuwatesa na kuwauwa. Matukio hayo hayawalengi waandamanaji tu, lakini pia waandishi wa habari, na majaji.