1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makampuni ya kidigitali kuanza kutekeleza sheria mpya za EU

6 Machi 2024

Makampuni makubwa ya kidigitali duniani yatalazimika kufuata sheria kali za Umoja wa Ulaya kuanzia Alhamis ya wiki hii, Umoja wa Ulaya unaamini kuwa sheria hizo mpya zitafanya soko la mtandaoni kuwa la haki kwa wote.

Social Media Apps | WhatsApp und Facebook
Majukwaa ya kidigitali kama Facebook, Whatsapp na mengineyo yanatarajiwa kuanza kufguata sheria mpya zilizokwekwa na Umoja wa UlayaPicha: Sebastian Kahnert/dpa/picture alliance

Makampuni makubwa ya kidigitali duniani yatalazimika kuchukua mkondo mpya wa kufuata sheria kali za Umoja wa Ulaya kuanzia Alhamis ya wiki hii, Umoja wa Ulaya unaamini kuwa sheria hizo mpya zitafanya soko la mtandaoni kuwa la haki kwa wote.

Septemba mwaka uliopita, Umoja wa Ulaya uliweka wazi sheria mpya 6 ambazo zinatazamiwa kuwa muongozo wa majukwaa 22 ya kidigitali yakiwemo Facebook, Instagram na LinkedIn ambayo lazima yafuate sheria hizo.

Soma zaidi: Wataalamu wataka gharama za huduma za intaneti kupunguzwa

Mitandao mingine inayopaswa kutekeleza hatua pia ni pamoja na mtandao wa Google, Amazon, Apple, TikTok, parent ByteDance, Meta na Microsoft.

Orodha nyingine itaongezwa hivi karibuni

Orodha hiyo inatarajiwa kuongezeka baada ya wakala wa usafiri wa mtandaoni wa Booking na mkuu wa mtandao wa X Elon Musk kuiarifu tume ya Ulaya wiki iliyopita kwamba mtandao wao pia umetimiza vigezo vya kujumuishwa katika sheria hiyo.

Afisa Mkuu Mtendaji wa mtandao wa kijamii wa X Elon MuskPicha: Gonzalo Fuentes/REUTERS

Kwa mujibu wa tume ya Umoja wa Ulaya ni kwamba Makampuni makubwa ya teknolojia hutengeneza faida ya mabilioni ya dola kila mwaka na athari ya matokeo yake ni kwamba makampuni madogo yanayochipukia hujikita kwenye kizuizi.

Hali hiyo inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu inayowapa mamlaka makubwa makampuni yaliosimama tayari kiuchumi kutumia mabavu kuwazima wapinzani wao wanaochipukia kabla ya kuwa tishio na washindani katika biashara yao ya mtandaoni.

Soma zaidi: Miaka 50 ya habari na teknolojia ya mawasiliano Kenya

Sasa katika sheria hii mpya masuala yote yanayohusu manunuzi ya mtandaoni, hata ukiwa mdogo kiasi gani, utalazimika kujulishwa kwa tume, kitengo cha utendaji cha Umoja wa Ulaya chenye makao yake makuu mjini Brussels, Tume hiyo pia itafanya kazi kama mdhibiti mkuu wa masuala ya ushindani miongoni mwa makampuni.

Hali ilikuwaje

Baada ya kashfa nyingi ambazo ziliukumba mtandao wa kijamii wa Facebook unaomilikiwa na kampuni ya Meta, watumiaji wengi walichagua kubadilisha huduma za ujumbe zao kwa kutumia Messenger au WhatsApp na badala yake wakahamia kutumia mtandao wa telegram na Signal.

Wamiliki wa mitandao na tovuti kubwa duniani, Jeff Bezos(Katikati), Elon Mask(Kushoto chini), Bernard Arnault(Kulia juu), Larry Ellison(Kushoto juu) na Warren Buffet(Kulia chini).Picha: La Nacion/ZUMA/picture alliance

Lakini pamoja na hayo, bado kampuni ya Meta inaonekana kuwa na nguvu zaidi katika soko la mtandaoni, na hivyo kufanya kuwa vigumu kwa wasiopenda mtandao kama wa WhatsApp kuacha kutuma ujumbe kwa familia na marafiki zao.

Kwa upande mwingine, kampuni ya Amazon ambayo ni jukwaa kuu la ununuzi kwa maelfu ya makampuni kuuza bidhaa zao mtandaoni nayo ilikabiliwa na tuhuma chungu nzima na kwamba inatumia vibaya jukumu lake kama soko ili kuweka bidhaa zake bora kama muuzaji reja reja.

Kwa msingi huo sasa sheria mpya ya Umoja wa Ulaya inapiga marufuku mgongano huu wa kimaslahi, pamoja na kuyataka makampuni hayo kuimarisha ufanisi wa matumizi ya mitandao kwa watumiaji na kuhakikisha usalama wao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW