Sheria mpya dhidi ya migomo yaanza kutumika Uingereza
2 Julai 2023Chini ya sheria hiyo mpya, polisi sasa inaweza kuwahamishia mahali pengine waandamanaji wanaosababisha usumbufu kwa vyombo vya usafiri. Katika sheria hiyo pia, waandamanaji watakaopatikana na hatia ya kuzuwia ujenzi wa miundombinu mipya wanaweza kukabiliwa na hukumu ya kifungo cha miaka mitatu jela.
Maandamano ya wanamazingira yamekuwa yakilaaniwa
Pamoja na hayo, mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kuzuia mradi mkubwa wa usafiri anaweza kufungwa jela kwa kipindi cha miezi sita. Mamlaka nchini humo mara kwa mara zimekuwa zikiyalaani maandamano ya wanamazingira wakiwemo wa makundi ya "Just stop oil na "Extinction Rebellion" ambao wanahamasishaji juu ya dharura ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kufanya maandamano makubwa kwenye barabara zenye magari mengi. Hata hivyo, wakosoaji wanasema sheria kali ni kitisho kwa haki ya kuandamana .